Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

SIMANZI! BIBI ALIYEMLEA SAM WA UKWELI AACHWA MPWEKE – VIDEO


INAHUZUNISHA SANA! Hivyo ndiyo unavyoweza kusema kufuatia kifo cha aliyekuwa msanii wa Bongo Fkleva, Sam wa Ukweli, Bibi aliyekuwa akimlea amebaki mpweke baada ya kumpoteza mjukuu wake huyo kipenzi aliyekuwa akimsaidia mambo mengi ikiwemo shida ndogondogo za maisha.

Bibi huyo alianza kumlea Sam tangu akiwa mtoto baada ya wazazi wake wote kufariki dunia akiwa angali mdogo. Alishi naye hadi kipindi alipoamua kwenda Dar es Salaam kutafuta maisha na kuanza harakati zake za muziki.

Licha ya kuishi Dar, Sam aliendelea kumkumbuka bibi yake na ikiwemo kumjengea nyumba ambayo ndiyo anaishi bibi huyo katika Kijiji cha Kiwangwa, Bagamoyo alikozaliwa, kulelewa na kukua msanii huyo.

Sam wa Ukweli alifariki dunia Jumatano usiku, Juni 6, 2018 katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu, na kuzikwa jana Ijumaa katika nyumbani kwao Kiwangwa, Bagamoyo, ambapo mazihsi yake yalihudhuriwa pia na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva wakiongozwa na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.

MTAZAME BIBI WA SAM WA UKWELI

 NA GPL

No comments: