Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

KANISA KATOLIKI LAHOJI UTAMBULISHO WA WAPENZI YA JINSIA MOJA

Uongozi wa makao makuu ya kanisa katoliki umetoa waraka wa mwongozo unaopinga dhana ya kisasa juu ya utambulisho wa jinsia.
Mwongozo huo wenye kurasa 31 za mafundisho, umetolewa ukiwa na kichwa cha taarifa ''Mungu aliumba Mke na mume''
Mwongozo huo unazungumzia "mzozo wa mafundisho" na kuongeza kuwa mjadala wa sasa kuhusu jinsia unaweza "kupotosha dhana asilia " ya jinsia na kuyumbisha familia.
Waraka huo ambao umetolewa wa wakati wapenziwa jinsia moja wakiendelea na sherehe za mwezi wa kujivunia jinsia zao , umekosolewa mara moja na makundi ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadilisha jinsia zao LGBT.
Viongozi wa kanisa katolikiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKanisa katoliki limesema jinsia ya mtu haimriwi na watu binafsi bali huamriwa na Mungu pekee na kwamba maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili , kazi ya mwanamme na mwanamke
Waraka huo wa kanisa katoliki umetolewa na kongamano la Katoliki la Elimu kama mwongozo wa mafunzo kwa wale wanaohusika na masuala ya watoto.
Waraka huo haukutiwa saini na Papa Francis mwenyewe, lakini uliinukuu kauli yake na maandiko ya biblia kuhusiana na jinsia zilizoumbwa na Mungu kulingana na kanisa katoliki.

Waraka unasemaje?

Waraka unatoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo, lakini unatoa mwongozo juu ya masuala kadhaa yakiwemo yanayohusu jamii ya watu wanaobadilisha jinsia yao.
Unakosoa vikali uelewa wa kisasa kuhusu jinsia na kulifanya suala la jinsia kuwa gumu kuliko ilivyo kawaida ambapo kuna wanaume na wanawake.
Waraka huo umeendelea kusema kuwa nadharia za kisasa "zinapinga maumbile halisi " na badala yake " linakuwa ni swala la hisia za binadamu ".
Waraka huo unasema pia kwamba utambulisho wa jinsia "mara nyingi hauna msoingi wowote isipokuwa ni dhana potofu ya mkanganyiko wa uhuru wa hisia za mtu na vile anavyotaka yeye kuonekana na kutambulika ".
2019 Wapenzi wa jinsia moja wakifanya matembezi yao wakiwa wamebeba mabango yaoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwongozo wa umetolewa wakati wapenzi wa jinsia moja wakisherehekea mwezi wa kujivunia jinsia yao
Waraka huo unaendelea kusema kuwa jinsia haiamriwi na watu binafsi bali huamriwa na Mungu pekee: " Maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili , kazi ya mwanamme na mwanamke ."
Wapenzi wa jinsia moja
Image captionWapenzi wa jinsia moja
Waraka huo unasema kuwa taasisi zinapaswa kufundisha jamii kwa usawa juu ya "asili ya kweli ya wanadamu"kwa kuzingatia "elimu ya historia na tabia ya maendeleo ya binadamu kwa uwazi na kwa njia inayoaminika ".
Wapenzi wa jinsia moja katika moja ya matembezi ya kujivunia jinsia zao. Matembezi haya hufanyika kila mwaka katika nchi mbali mbali hususan za magharibi
Image captionWapenzi wa jinsia moja katika moja ya matembezi ya kujivunia jinsia zao. Matembezi haya hufanyika kila mwaka katika nchi mbali mbali hususan za magharibi
Hata hivyo, waraka huo unasema kwamba waoto na vijana wanapaswa kufundishwa kumuheshimu kila mtu ili asiwepo hata mmoja atakayeumizwa na matusi au ubaguzi wa aina yoyote ile
Kundi la New Ways, lenye makao yake nchini Marekani ambalo linatetea wapenzi wa jinsia moja Wakatoliki, limeelezea waraka huo wa kanisa katoliki kama '' zana hatari'' ambayo itatumiwa "kuwadunisha na kuwadhuru watu waliobadilisha jinsia zao, pamoja na wapenzi wa jinsia moja wakike na wakiume ".
  • Mkurugenzi New Ways- Francis DeBernardo, amepinga vikali dhana kuwa watu "huchagua jinsia zao".
Katika taarifa iliyojibu waraka wa kanisa katoliki ,Francis DeBernardo , alisema kuwa waraka huo ''utawakanganya wale wanaohangaika kutafuta jinsia yao " na akaelezea kuwa Vatican imekuwa "katika kipindi cha giza " kuhusiana na suala la utambulisho wa jinsia.

bbcswahili

No comments: