NDALICHAKO, ANNA MGHWIRA WAHUDHURIA MAZISHI YA AKWILINA ROMBO
Mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umewasili katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambako inafanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu.
Baada ya ibada hiyo ndugu, jamaa, viongozi na watu wa kada mbalimbali watatoa heshima za mwisho na kisha mwili kupelekwa nyumbani kwa ajili ya mazishi yatakayoanza saa saba mchana.
No comments: