MAWAZIRI WATATU WATAKIWA KUMALIZA MKWAMO WA AJIRA NCHINI
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 10, 2018, Katibu wa Sera na Tafiti wa Ngome ya vijana wa chama hicho, Kitentya Luth amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kushuhudia wimbi la waajiri sekta binafsi na Serikali kupunguza wafanyakazi.
"Hata sekta ya elimu na viwanda ambazo awali zilikuwa zinatoa ajira nyingi nazo hali ni mbaya. Walimu hawajapata ajira kwa zaidi ya miaka mitatu, jambo hilo linasababisha mkwamo katika elimu lakini pia vijana hao wanashindwa kujikwamua kimaisha," amesema Luth.
No comments: