POLISI: ATAKAYEANDAMANA ASITULAUMU
Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa kikundi kinachohamasisha maandamano kupitia mtandao wa Telegramna kusema litafanya kila liwezekanalo kisheria kukizuia.
Hatua kali kuchukuliwa kwa wanaohusika na makundi hayo kwani kitendo hicho ni sawa na uhaini kwa kuwa wanataka kuiangusha Serikali. Jeshi limesema lisije likalaumiwa baadae.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operation na mafunzo, CP Nsato Marijani alipokuwa amekutana na wanahabari kwa maagizo ya IGP Sirro kuwa Jeshi la Polisi linatakiwa kutoa habari ya matukio kwa kila kipindi cha mwezi mmoja.
Aidha, Jeshi limesema Matukio ya mauaji yamepungua hadi kufikia matukio 235 kwa kipindi cha Januari 2018, kutoka matukio 288 Januari 2017 pungufu ya matukio 53 sawa na 18.%.
Matukio ya kubaka yamepungua hadi kufikia matukio 588 Januari 2018 kutoka matukio 732 Januari 2017 pungufu ya matukio 144 ni sawa na 19.7%.
No comments: