Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

SAKATA LA TICHA AYUBU WA ST FLORENCE, MSIMAMO WA SERIKALI NI HUU – VIDEO

WAZIRI wa Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametoa onyo kali kwa walimu wenye tabia kama aliyoionesha mwalimu Ayubu wa St Florence ya jijini Dar es Salaam.

Ndalichako amesema serikali haiwezi kuvumilia kuwa na walimu wa aina hiyo lakini pia serikali haiwezi kuzivumilia shule ambazo hazizingatii usalama wa wanafunzi wawapo shuleni.

Akaongeza kwamba suala la wanafunzi waliodhalilishwa katika Shule ya St. Florence, linafuatiliwa kwa karibu na serikali na kwamba uchunguzi utakapokamilika, hatua kali zitachukuliwa ili kukomesha tabia za udhalilishaji kwa wanafunzi.
NA GPL

No comments: